Friday, October 3, 2014

TLIMUUZA ROJO KWA SHINIKIZO - RAIS.

RAIS wa klabu ya Sporting Lisbon, Bruno de Carvalho amedai kuwa walikuwa chini ya shinikizo kutoka nje ili wamuuze Marcos Rojo kwenda Manchester United. De Carvalho amesema wamiliki wa tatu alihudhuria mikutano yao na kuwafanya waamini kuwa ni maofisa wa United. Rais huyo alidai kuwa walikuwa hawana mpango wa kumuuza Rojo kwakuwa alikuwa mchezaji muhimu kwao. Beki huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 24 ambaye alijiunga na Sporting Lisbon mwaka 2012 alisajiliwa na United kwa kitita cha paundi milioni 16. De Carvalho amesema shinikizo lilikuwa kubwa sana kwani watu walianza kuongeza na klabu na kwenda huko kwa ajili ya mikutano. Umiliki wa tatu wa mchezaji umefungiwa nchini Uingereza hivyo inamaanisha timu yoyote katika Ligi Kuu inayotaka kununua mchezaji wa aina hiyo wanapaswa kuwanunua kwanza wamiliki wowote wengine.

No comments:

Post a Comment