Friday, October 3, 2014

UNITED WAJIHAMI YASIWAKUTE YA TEVEZ KWA KUMALIZANA KABISA NA FALCAO.

KLABU ya Manchester United tayari imeshakubali masuala binafsi yaliyopendekezwa katika usajili wa kiangazi kwa Radamel Falcao ili kuepusha kilichotokea kwa Carlos Tevez miaka mitano iliyopita. United ilimsajili mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Colombia kwa mkopo akitokea Monaco katika siku ya mwisho ya usajili wa kiangazi hiki. Wakiwa wamelipa ada ya paundi milioni sita kwa Monaco kwa ajili ya mkopo wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 28, United pia walikubali kutoa kitita cha paundi milioni 43 kama wakiamua kumsajili moja kwa moja mshambuliaji huyo mwishoni mwa msimu. Sasa inaonekana kuwa Ofisa Mkuu wa United Ed Woodward tayari wameshakubaliana na mchezaji huyo kumlipa mshahara wa paundi 250,000, marupurupu na haki za kutumia picha yake kama wakiamua kumchukua moja kwa moja msimu ujao. United imefanya hivyo ili kuepuka yaliwakuta kwa Tevez mwaka 2009 ambapo walikubali kumchukua kwa paundi milioni 25 baada ya kumtumia kwa mkopo msimu miwili lakini dili hilo lilishindikana baada ya kushindwa kufikia makubaliano binafsi na kupelekea nyota huyo kwenda kwa mahasimu wao Manchester City.

No comments:

Post a Comment