Thursday, October 16, 2014

IBRAHIMOVIC BADO GONJWA - BLANC.

MSHAMBULIAJI nyota wa Paris Saint-Germain-PSG, Zlatan Ibrahimovic bado hajapona sawasawa majeruhi yaliyokuwa yakimsumbua hivyo kumfanya kuondolewa katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Ufaransa utakaochezwa kesho dhidi ya RC Lens. Hayo yamesemwa na kocha wa timu hiyo Laurent Blanc katika mkutano na wanahabari leo ambapo amedai kuwa nyota huyo yuko katika hatua nzuri lakini bado hayuko tayari kufanya mazoezi na kikosi kucheza. kwa mujibu wa kocha huyo beki wake wa kati Thiago Silva amerejea baada ya kupona majeruhi ya msuli ambayo yalimuweka nje toka katikati ya mwezi ya Agosti mwaka huu. Ibrahimovic hajaichezea klabu wala nchi yake ya Sweden kwa karibu wiki nne toka alipoumia katika mchezo dhidi ya Olympique Lyon ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1. PSG ambao hawajafungwa msimu huu wako katika nafasi ya tatu wakiwa na alama 15 katika michezo tisa waliyocheza, wakitofautiana alama saba na vinara Olympique Marseille.

No comments:

Post a Comment