Thursday, October 16, 2014

RONALDO AWEKA REKODI NYINGINE KWA KUWA MCHEZAJI SOKA WA KWANZA KUFIKISHA LIKES 100 FACEBOOK.

MSHAMBULIAJI mahiri wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Real Madrid ameendelea kung'aa sio ndani ya uwanja lakini hata nje ya uwanja kwa kuwa mchezaji wa kwanza kufikisha idadi ya mashabiki milioni 100 ambao wame-like ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook. Ronaldo ambaye ni mshindi mara mbili wa tuzo wa Ballon d'Or msimu huu ameanza vyema kwani ameshafunga mabao 18 katika mechi 14 za mashindano yote alizocheza mpaka sasa. Nyota mwingine anayemfuata kwa karibu kwa kuwa na Likes nyingi katika mtandao huo ni wanamuziki Shakira, Eminem na Rihanna. Ronaldo alitengeneza video fupi ya kuwashukuru mashabiki wake popote walipo na kudai kuwa hiyop ni hatua kubwa kwao na kwake. Wachezaji soka wengine wanaomfuata kwa karibu Ronaldo, ni nyota wa Barcelona Lionel Messi mwenye idadi ya Likes milioni 74.

No comments:

Post a Comment