Saturday, October 18, 2014

CAVANI ALIMWA NYEKUNDU AKISHANGILIA.

MSHAMBULIAJI wa Paris Saint-Gemain-PSG, Edinson Cavani alijikuta akitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa ya kushangilia kwa kuonyesha ishara ya mtutu wa bunduki na kulalamika kwa mwamuzi wakati timu hiyo ilipoifunga Lens. Bao la umbali wa mita 20 lililofungwa na Adama Coulibaly liliipa uongozi Lens lakini Yohane Cabaye alisawazisha kabla ya Maxwell kuongeza la pili kwa PSG huku Jean-Philippe Gbamin akitolewa nje kwa kumchezea vibaya Cavani katika eneo la hatari. Cavani alifunga bao lapenati ambalo lilikuwa la tatu na kupewa kadi ya njano kwa kushangilia akionyesha ishara yam tutu wa bunduki kabla ya kuongezwa kadi nyingine ya njano kwa kumshika mwamuzi Nicolas Rainville mkono kulalamika kadi ya kwanza aliyopewa. Cavani ambaye alisajiliwa kutoka Napoli kwa kitita cha paundi milioni 55 Julai mwaka jana, ndiye mshambuliaji wa kutegemewa wa PSG kwasasa wakati Zlatan Ibrahimovic akiendelea kujiuguza majeruhi. Rais wa PSG Nasser Al Khelaifi amesema haoni kama Cavani alistahili kadi nyekundu kwani mara zote amekuwa akishangilia namna hiyo pindi afungapo bao.

No comments:

Post a Comment