Saturday, October 18, 2014

MOURINHO AWASHANGAA FA KWA KUYOMUADHIBU WENGER.

MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho anaamini kushindwa kwa Chama cha Soka cha Uingereza-FA kumuadhibu Arsene Wenger kwa kumsukuma kinawaacha katika hatia na kusisitiza kuwa kama ingekuwa yeye ndiye aliyefanya tukio hilo wasingesita kumfungia. Kufuatia kuchezewa vibaya Alexis Sanchez na Gary Cahill wakati wa mchezo Chelsea walioshinda mabao 2-0 dhidi ya Arsenal mapema mwezi huu, Wenger alivamia eneo la Mourinho kulalamikia faulo hiyo na kumsukuma Mreno huyo wakati akimwambia arejee eneo lake. Akihojiwa Mourinho amesema ameshangazwa kwa Wenger kutoadhibiwa na FA kwa kitendo chake hicho kwani anaamini ingekuwa yeye lazima angechukuliwa hatua. Wenger mwenyewe tayari aliomba radhi kwa tukio hilo na kudai kuwa alichokuwa akilalamikia ni kuchezewa faulo mchezaji wake na sio vinginevyo.

No comments:

Post a Comment