Saturday, October 18, 2014

STURRIDGE APATA MAJERUHI MENGINE.

MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Daniel Sturridge anakabiliwa na kuendelea kukaa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu zaidi baada ya kupata majeruhi mengine akiwa mazoezini. Sturridge mwenye umri wa miaka 25 ndio alikuwa kwanza amepona majeraha ya msuli aliyopata mwezi uliopita wakati akiitumikia Uingereza. Nyota huyo amecheza mechi tatu pekee za Ligi Kuu msimu huu na anaweza kukosa mechi zingine saba ukiwemo mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid. Meneja wa Liverpool, Brendan Rodgers amesema taarifa hizo zimekuwa pigo kubwa kwani atakuwa nje ya uwanja tena kwa kipindi wiki mbili mpaka nne. Sturridge ambaye alifunga mabao 25 katika mashindano yote msimu uliopita alikuwa akitegemewa kurejea uwanjani kesho katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Queens Park Rangers.

No comments:

Post a Comment