WINGA mahiri wa klabu ya Arsenal Theo Walcott alicheza kwa dakika 45 katika kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 21 cha timu hiyo dhidi ya Blackburn Rovers ikiwa ni dalili njema za kurejea katika kikosi cha kwanza baada ya kupona majeruhi ya goti. Walcott amekaa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi tisa baada ya kuchanika msuli wa ndani wa goti lake la kushoto wakati mchezo wa mzunguko wa tatu wa Kombe la FA dhidi ya Tottenham Hotspurs Januari mwaka huu. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 alikosa fainali ya michuano hiyo dhidi ta Hull City sambamba na michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika nchini Brazil. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo uliomalizika kwa sare ya bila kufungana, Walcott amesema miezi tisa aliyokaa nje ilikuwa ni migumu kwake kwani mara zote amekuwa akitaka kucheza na kuonyesha uwezo wake. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa ataendelea kuwa mvumilivu mpaka hapo kocha atakapoona wakati umefika kwake kuwemo katika kikosi cha kwanza.

No comments:
Post a Comment