Saturday, October 18, 2014

BARTOMEU KUGOMBEA TENA URAIS BARCELONA.

RAIS wa klabu ya Barcelona, Josep Maria Bartomeu amethibitisha mipango yake ya kugombea tena nafasi hiyo wakati kipindi chake sasa kitafikia ukingoni. Bartomeu mwenye umri wa miaka 51 alishika wadhifa huo akichukua nafasi ya Sandro Rosell aliyejiuzulu Januari mwaka huu kufuatia utata wa usajili wa Neymar kutoka klabu ya Santos. Baadhi ya wadau walikuwa wkaitaka kuitishwa kwa uchaguzi mpya baada ya kuondoka Rosell lakini Bartomeu aliyecchukua nafasi hiyo amesema suala hilo litafanyika pindi atakapomaliza muda wake ambao ni Juni 30 mwaka 2016. Bartomeu amesema toka amechukua madaraka hayo amekuwa akipata changamoto nyingi wakiwemo watu kumkosoa lakini amekuwa mvumilivu na kusikiliza kasha kuyafanyia kazi malalamiko yao.

No comments:

Post a Comment