Saturday, October 18, 2014

NYOTA WA BRAZIL AKABILIWA NA ADHABU KWA KUJIVUTA JEZI KUMDANGANYA MWAMUZI.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Brazil, Leandro Damiao anakabiliwa na kifungo cha miezi sita kutoka katika mahakama ya michezo ya nchi hiyo-STJD kwa kujivuta shati mwenyewe ili aweze kupata penati. Nyota huyo wa klabu ya Santos alijivuta shati lake wakati akikimbia mbele kufuata mpira wa kona wakati wa mchezo dhidi ya Criciuma ambao walichapwa mabao 3-0. Ingawa mwamuzi hakuona tukio hilo STJD wameamua kumshitaki nyota huyo kwa tukio lisilo la uanamichezo baada ya kupata ushahidi wa picha za video. Kwa mujibu wa sheria za soka za Brazil, mchezaji yeyote aataegundulika kutaka kumdanganya mwamuzi kwa makusudi atakabiliwa na adhabu ya kufungiwa mechi zisizopungua sita.

No comments:

Post a Comment