Tuesday, October 21, 2014

KIONGOZI ATOA WAZO LA MECHI ZA QATAR KUCHEZWA USIKU WA MANANE.

MECHI za Kombe la Dunia nchini Qatar zinaweza kumalizika usiku wa manane mpaka saa tisa alfajiri kama mapendekezo yaliyotolewa na ofisa wa ngazi juu katika soka yatafanyiwa kazi. Harold Mayne-Nicholls ambaye anatarajiwa kumpa changamoto Sepp Blatter katika kinyang’anyiro cha urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA mwakani, amesema michuano hiyo ya mwaka 2022 bado inawezekana kufanyika katika majira ya kiangazi. Lakini Ofisa huyo wa zamani wa soka wa Chile amesema baadhi ya michezo italazimika kuanza usiku mkubwa ili kuepuka joto kali. Mayne-Nichollos aliendelea kudai kuwa inawezekana mchezo wa kwanza ukachezwa saa moja za usiku, wa pili saa nne na mchezo wa tatu ukaanza saa saba za usiku. Inategemewa michuano hiyo ya Qatar kuhamishwa katika majira ya baridi ili kuepuka joto kali huku FIFA wakifikiria kuipeleka Novemba na Desemba lakini Mayne-Nicholls amesema kufanya hivyo kutavuruga ratiba ya ligi mbalimbali duniani. Qatar walipewa uenyeji wa kuandaa michuano hiyo ya mwaka 2022 na kamati ya utendaji ya FIFA mwaka 2010.

No comments:

Post a Comment