Monday, October 20, 2014

MOURINHO AMCHANA DEL BOSQUE KUHUSU COSTA.

MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amekosoa huduma ya baadhi ya wachezaji wake katika majukumu ya kimataifa baada ya kubainisha kuwa Diego Costa anatarajiwa kukoa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Maribor kesho. Mourinho alithibitisha Costa ambaye pia alikosa mchezo wa mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya Crystal Palace walioshinda mabao 2-1 kutonesha majeruhi ya msuli wa paja wakati akiitumikia Hispania katika mechi dhidi ya Slovakia na Luxembourg. Kocha huyo amesisitiza kutokuwa na mawasiliano na kocha wa timu ya taifa ya Hispania au madaktari wa timu hiyo kuhusu hali ya Costa kabla mchezaji huyo hajajiunga nao. Mourinho amedai Costa anasumbuliwa na tatizo lilelile na anadhani kama wangewasiliana mapema na Del Bosque na kuzungumzia hali ya mchezaji huyo anadhani mambo yangekuwa tofauti.

No comments:

Post a Comment