Thursday, October 16, 2014

LE ROY KUMPELEKA MASHABA FIFA.

KOCHA wa timu ya taifa ya Congo Brazaville, Claude Le Roy amemtuhumu kocha wa timu ya taifa ya Afrika Kusini Shakes Mashaba kwa kumuonyesha ishara chafu katika mchezo wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika baina ya timu hizo uliochezwa jana huko Polokwane. Le Roy ambaye kikosi chake kiligawana alama na Bafana Bafana kwa kutofungana katika Uwanja wa Peter Mokaba, ametishia kumshitaki Mushaba Shirikisho la Soka Duniani-FIFA na Shirikisho la Soka Afrika-CAF kwa ishara hiyo ambayo hawezi kuirudia mbele ya wanawake. Akihojiwa kocha huyo amesema ameshangazwa na tabia Mashaba mwishoni mwa mchezo huo kwa kumuonyesha ishara hiyo chafu kwani ni mara ya kwanza katika miaka yake 34 ya ufundishaji soka kukutana na kitendo hicho. Le Roy amesema wana ushahidi wa picha kutoka kwa mmoja wa wapiga picha wao na anadhani FIFA na CAF watapelekewa picha hiyo kwasababu kocha msomi huwezo kukubaliana na tabia kama hizo.

No comments:

Post a Comment