Thursday, October 16, 2014

SERBIA, ALBANIA HATARINI KULIMWA ADHABU NA UEFA KWA VURUGU.

VYAMA vya Soka vya nchi za Serbia na Albania vimeshitakiwa na Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA baada ya matukio ya vurugu yaliyopelekea mchezo wao wa kufuzu michuano ya Ulaya 2016 kusimamishwa. Wachezaji na mashabiki walivamiana jijini Belgrade baada ya bendera iliyokuwa na ujumbe wa siasa kupitishwa uwanjani na ndege isiliyokuwa na rubani. Albania wao wameshitakiwa kwa kugoma kuendelea kucheza na kupitisha bendera hiyo iliyozua zogo wakati Serbia wao wanakabiliwa na makosa matano yanayohusiana na vurugu za mashabiki. Kamati ya maadili na nidhamu ya UEFA inatarajiwa kuanza kusikiliza kesi hiyo Octoba 23 mwaka huu. Tukio hilo limelaaniwa vikali na viongozi wa soka akiwemo rais wa Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA Sepp Blatter ambaye alidai kuwa soka halitakiwi kuhusishwa na masuala ya kupeleka ujumbe wa kisiasa.

No comments:

Post a Comment