MABAO manne yaliywekwa kimiani na Neymar yameisaidia Brazil kupata ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Japan leo mchana katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa huko Singapore. Kocha wa Brazil, Dunga anaendeleza wimbi lake la ushindi toka achukue mikoba hiyo kwa mara ya pili kutoka kwa Luiz Felipe Scolari aliyetimuliwa kutokana na timu kushindwa kufanya vyema katika Kombe la Dunia walilokuwa wenyeji. Dunga ambaye amewahi kushinda taji la Kombe la Dunia akiwa nahodha wa Brazil mwaka 1994, huo unakuwa ushindi wan ne mfululizo kupata bila timu hiyo kuruhusu bao. Jumamosi iliyopita Brazil iliitandika Argentina waliokuwa washindi wa pili katika Kombe la Dunia kwa mabao 2-0 katika mchezo mwingine wa kirafiki uliofanyika jijini Beijing, China.

No comments:
Post a Comment