Tuesday, October 14, 2014

SUAREZ AKIRI ILIKUWA NGUMU KUKUBALI UKWELI WA KUMNG'ATA CHIELLINI.

MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Luis Suarez amesema ilikuwa ngumu kukubaliana na ukweli wa kumng’ata beki wa Italia Giorgio Chiellini katika michuano ya Kombe la dunia nchini Brazil. Nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay ambaye alijiunga na Barcelona akitokea Liverpool kwa kitita cha paundi milioni 75 alifungiwa miezi minne kutokana na tukio hilo. Akihojiwa Suarez amesema alikuwa akiona vigumu kukubali alichokifanya kwani yeye ni binadamu kama walivyo wengine. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 amesema likuwa hataki kumsikiliza yeyote au kuongeza na yeyote kwasababu alikuwa hataki kukubaliana na ukweli. Suarez alimuomba radhi Chiellini Juni 30 zikiwa zimepita siku sita toka afanye tukio baada ya Uruguay kushinda bao 1-0 dhidi ya Italia, msamaha ambao ulipokelewa na beki huyo na kueleza matumaini yake kama Shirikisho la Soka Duniani-FIFA lingeweza kumpunguzia adhabu hiyo. Kabla kuomba radhi Suarez alikanusha kwa kudai kuwa aliteleza bahati mbaya na uso wake kumuangukia Chiellini jambo ambalo lilikuwa kama vichekesho kwani tukio hilo lote lilionekana katika picha za video.

No comments:

Post a Comment