Tuesday, October 14, 2014

ARSENAL ITAKABILIWA NA CHANGAMOTO KUBWA AKIONDOKA WENGER - GIZADIN.

OFISA mkuu wa Arsenal, Ivan Gazidin amedai kuwa klabu hiyo itakabiliwa na changamoto kubwa kutafuta mbadala wa meneja Arsene Wenger wakati atakapoamua kuondoka. Wenger ambaye anatimiza miaka 65 Octoba 22 mwaka huu, alisaini mkataba mpya wa miaka mitatu Mei. Gazidin amesema Changamoto kubwa itakayowakabili kama klabu ni mabadiliko kutoka Wenger kuelekea kwa meneja mpya. Arsenal imefanikiwa kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mara 17 mfululizo chini ya Wenger na Mfaransa huyo alioongoza klabu hiyo kushinda taji lake la kwanza baada ya kupita miaka tisa wakati waliponyakuwa taji la FA Mei mwaka huu. Wenger aliteuliwa kuinoa Arsenal mwaka 1996 akiwa hajulikani kabisa na kufanikiwa kuingoza timu hiyo kunyakuwa taji la Ligi Kuu mwaka 1997-1998, 2001-2002 na 2003-2004.

No comments:

Post a Comment