NIGERIA imepewa hadi Ijumaa kubadili msimamo wake kuhusu uamuzi wa mahakama iliyotupilia mbali uchaguzi wa viongozi wa Shirikisho la Soka nchini humo-NFF kabla ya FIFA kuwafungia kushiriki michuano ya kimataifa hadi Mei mwakani. Kwa mujibu wa barua iliyotumwa kwa NFF, agizo hilo la FIFA ni sharti litimizwe kufikia mchana wa tarehe 31 October. FIFA inataka bodi iliyochaguliwa Septemba 30 mwaka huu kurejeshwa madarakani haraka. Kama Nigeria ikifungiwa itapoteza nafasi ya kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika ambapo wao ni mabingwa watetezi. Tayari Nigeria imeshapigwa marufuku mara mbili mwaka huu kutokana na hatua ya serikali kuingilia masuala ya soka.
No comments:
Post a Comment