MWANARIADHA nyota mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amerejea tena mahakamani leo kusikiliza hukumu yake baada ya kushitakiwa kwa kosa la kumuua la mpenzi wake Reeva Steenkamp. Pistorius alikutwa na hatia ya kuua bila kukusudia mwezi uliopita baada ya jaji Thokozile Masipa kudai kuwa upande mashitaka ulishindwa kuthibitisha kwamba mwanariadha huyo aliua kwa kukusudia. Jaji Masipa anategemea kusikiliza hoja za kisheria na ushahidi kwa siku kadhaa kabla ya kutoa hukumu yake rasmi. Pistorius anakabiliwa na kifungo cha miaka 15 jela, ingawa jaji Masipa anaweza kubadilisha kifungo hicho na kumtoza faini mtuhumiwa.

No comments:
Post a Comment