Monday, October 13, 2014

LIGI KUU INDIA YAZINDULIWA RASMI.

LIGI Kuu ya Soka nchini India ijulikanayo kama Indian Super League imeanza rasmi jana huku timu ya Mumbai City ikichabangwa kwa mabao 3-0 na Atletico de Kolkata. Nahodha wa zamani wa kriketi wa India Sachin Tendulkar, mmiliki mwenza wa timu mojawapo katika ligi hiyo Kerala Blasters waliokuwa miongoni mwa watu mashuhuri waliohudhuria ufunguzi wa ligi hiyo huko Calcuatta. Wachezaji wa Mumbai Nicolas Anelka na Freddie Ljungberg walikosa mchezo huo kutokana na majeruhi yanayowasumbua. Mabao katika mchezo huo yalifungwa na Fikru Teferra, Borja Fernandez na Arnal Llibert ambapo nyota wa zamani wa Liverpool Luis Garcia alikuwa akiichezea Kolkata. Ligi hiyo inatarajiwa kudumu kwa muda wa wiki 10, ikishirikisha timu nane kwa madhumuni ya kuibua umaarufu wa mchezo huo katika nchi hiyo ambayo imetawaliwa kwa kiasi kikubwa na kriketi.

No comments:

Post a Comment