KOCHA wa timu ya taifa ya Nigeria, Stephen Keshi bado yuko katika mshangao kufuatia kipigo walichopata kutoka kwa Sudan katika mchezo wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika. Nigeria wanajulikana kama Super Eagles walishindwa kucheza kwa kiwango chao cha juu na kujikuta wakichapwa bao 1-0 katika Uwanja wa Manispaa jijini Khartoum. Keshi amesema kikosi chake kingeweza kuibuka na ushindi katika mchezo huo kama nafasi walizotengeneza zingetumika ipasavyo lakini haraka aliwaomba radhi mashabiki wan chi hiyo kwa kupoteza mchezo huo. Keshi amesema inabidi aombe radhi kwani mashabiki wa Nigeria walikuwa na imani kubwa na timu yao kuibuka na ushindi. Mbali na Keshi lakini pia golikipa na nahodha wa Super Eagles Vincent Enyeama naye aliwaomba radhi mashabiki kwa kipigo hicho na niaba ya wachezaji wenzake na kuahidi kufanya vyema katika michezo yao inayofuata.

No comments:
Post a Comment