Monday, October 13, 2014

KOCHA WA ALGERIA ATAMBA KUNYAKUWA TAJI LA AFCON MWAKANI.

KOCHA wa timu ya taifa ya Algeria, Christian Gourcuff anaamini kikosi cha kinachojulikana kama Desert Foxes kiko katika kiwango kizuri cha kunyakuwa taji la michuano ya mataifa ya Afrika-AFCON itakayofanyika mwakani nchini Morocco. Kocha huyo amesema baada ya kiwango kizuri walichoonyesha katika Kombe la Dunia nchini Brazil sasa wanahitaji kufuzu fainali hizo za AFCON na pia kushinda taji lake mwakani. Algeria walishinda mchezo wao dhidi ya Malawi kwa mabao 2-0 na kubakia kileleni mwa kundiB wakiwa na alama tisa kutokana na michezo mitatu waliyocheza na wanapewa nafasi ya kushinda wakati watakapokwaana na Malawi tena Jumatano hii. Mabao yaliyofungwa na Rafik Halliche na Djamel Mesbah yalitosha kuwapa ushindi Algeria katika mchezo wao uliochezwa Jumamosi iliyopita katika Uwanja wa Kamuzu jijini Blantyre. Malawi wao wana alama tatu katika michezo mitatu waliyocheza na wako katika nafasi ya tatu huku Mali wakishika nafasi ya pili baada ya kuitandika Ethiopia inayovuta mkia kwa mabao 2-0.

No comments:

Post a Comment