MWENYEKITI wa klabu ya Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge anadhani Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA limehakiki jinsi gani walivyo makini na suala la Matumizi ya Fedha kwa kuiadhibu klabu ya Paris Saint-Germain-PSG. Mabingwa hao wa Ufaransa walitandikwa na faini ya euro milioni 60 na kulazimishwa kupunguza matumizi yao kwa msimu inayokuja wakati pia kikosi chao cha Ligi ya Mabingwa Ulaya kimepunguzwa wachezaji wane kutokana na kukiuka sheria hiyo mpya. Mabingwa wa Ligi Kuu Manchester City nao walilimwa adhabu kama hiyo wakati vilabu vingine vikiwemo Inter Milan, Liverpool na Monaco vimetakiwa kupeleka taarifa zao za matumizi ya fedha kwa msimu wa 2012-2013. Rummenigge ambaye pia ni kamu mwenyekiti wa Chama cha Vilabu barani Ulaya-ECA ana uhakika hatua hiyo iliyochukuliwa na UEFA ni nzuri kwa mustakabali wa soka la Ulaya. Kiongozi huyo amesema ni jambo jema kwa UEFA kutaka vilabu kukua taratibu badala ya ghafla kwa hela nyingi za wafadhili kwani zinahatarisha mustakabali wake.

No comments:
Post a Comment