Monday, October 13, 2014

AC MILAN YAKANUSHA ESSIEN KUUGUA EBOLA.

KLABU ya AC Milan imekanusha taarifa kuwa kiungo wa kimataifa wa Ghana Michael Essien ameambukizwa ugonjwa wa Ebola wakati akiwa katika majukumu ya kimataifa. Taarifa zilizozagaa nchini Ghana mwishoni mwa wiki iliyopita zimedai kuwa Essien alikuwa akipatiwa matibabu baada ya kuambukizwa virusi hivyo hatari. Hata hivyo klabu hiyo ya Serie A ilitoa taarifa kukanusha taarifa hizo na kudai kuwa hazina ukweli wowote na hazijawahi kuthibitishwa na mwajiriwa wao yeyote. Magazeti ya Daily Times na Newswire yote ya Nigeria yalitoa taarifa iliyothibitishwa na AC Milan ambayo inadai kuwa Essien aliambukizwa Ebola. Naye Essien mwenyewe alituma picha katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa instagram na kudai kuwa yuko fiti na mwenye afya tele na kukanusha tetesi zote zinazomhusisha yeye kupata ugonjwa hatari. Essien aliongeza kuwa virusi vya Ebola sio jambo la mzaha hivyo watu wanapaswa kutofanya utani na suala hilo.

No comments:

Post a Comment