NGULI wa soka wa Uholanzi, Johan Cruyff amedai kuwa Luis Suarez atawarejesha katika ubora wao Lionel Messi na Neymar. Suarez aliyesajiliwa na Barcelona kwa kitita cha euro milioni 88 kutoka Liverpool, bado hajacheza mchezo wowote kutokana na kutumikia adhabu ya miezi minne kwa kosa la kumng’ata beki wa Italia Giorgio Chiellini katika mchezo wa Kombe la Dunia kati ya Uruguay na Italia. Hata hivyo, Cruyff amesema ujio wa Suarez utakamilisha safu ya ushambuliaji ya timu hiyo na kuifanya iwe ya kuogopewa duniani. Akihojiwa Cruyff mwenye umri wa miaka 67 amesema anaamini kuwa uwepo Suarez unaweza kuimarisha muunganiko kati ya Messi na Neymar.

No comments:
Post a Comment