MCHEZO wa kirafiki wa kimataifa kati ya Brazil na Argentina utakaochezwa nchini China kesho uko katika tishio kwasababu ya wingu zito lililotanda jijini Beijing. Wachezaji wamelazimika kujifungia katika vyumba vyao baada ya mamlaka zinazohusika kutoa tahadhari ya moshi wenye rangi ya machungwa unaotokana na uchafuzi wa mazingira. Mpaka kufikia jana hali ya hewa katika jiji hilo ilikuwa mbaya mara 18 kuliko inavyotakiwa kuwa. Daktari wa timu ya Brazil, Rodrigo Lasmar amesema wachezaji wote wanalazimika kujifungia vyumbani mwao na kutoka wakati wa mazoezi hivyo kufanya kuwa kila muda wa saa 24 wao wanakuwa ndani kwa saa 22. Mechi hiyo ya kukata na shoka inawajumuisha nyota wa Argentina kama Lionel Messi, Angel Di Maria, Marcos Rojo, Martin Demichelis, Pablo Zabaleta na Sergio Ramos wakati Brazil kutakuwa na kina Willian, Oscar, Filipe Luis, Philippe Coutinho na Neymar.

No comments:
Post a Comment