Wednesday, October 8, 2014

UEFA YAMUADHIBU TAVACCHIO KWA UBAGUZI.

RAIS wa Shirikisho la Soka la Italia-FIGC, Carlo Tavacchio amefungiwa miezi sita na Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA kwa kutoka matamshi ya kibaguzi. Rais huyo mwenye umri wa miaka 72 alisababisha utata wakati wa kampeni zake za uchaguzi Julai mwaka huu kwa kuwafanisha wachezaji wa kigeni na wanaokula ndizi, ingawa baadae aliomba radhi kwa kauli hiyo. Adhabu hiyo aliyopewa inamaanisha Tavecchio hatakuwa na uwezo wa kushikilia nafasi yoyote ya UEFA na pia atafungiwa kuhudhuria mkutano mkuu wa shirikisho hilo Machi mwaka 2015. Tavecchio hatakuwa na uwezo wa kufanya majukumu yake kama mjumbe wa kamati ya vijana ya UEFA na pia ametakiwa na shirikisho hilo kuandaa tukio nchini Italia ili kuhamasisha vita dhidi ya ubaguzi wa rangi. Tavecchio alichaguliwa kushika nafasi hiyo katika uchaguzi wa Agosti kwa kumshinda mchezaji wa zamani wa AC Milan Demetrio Albertini hatua ambayo ilikosolewa na wadau wengi kutokana na kauli yake.

No comments:

Post a Comment