KOCHA wa zamani wa klabu ya Barcelona, Johan Cruyff amedai kiwango kibovu cha Mario Balotelli anachoonesha katika klabu ya Liverpool kinatokana na ukosefu wa elimu ya kutosha. Balotelli alijiunga na Liverpool kwa kitita cha euro milioni 20 akitokea AC Milan katika majira ya kiangazi msimu huu lakini mpaka sasa hajafunga bao katika Ligi Kuu huku mabao mawili aliyofunga yalitokana na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Ludogoret na Swansea City katika Kombe la Ligi. Kushindwa kwake kufunga kumewafanya watu wengi wahoji uwezo wake lakini Cruyff anaamini makosa yote sio ya Balotelli pekee kwasababu hakufundishwa tabia njema katika umri mdogo. Cruyff amesema kama nyota huyo angepata malezi na kufunzwa vyema asingeweza kuyafanya anayofanya hivi sasa.
No comments:
Post a Comment