SHIRIKISHO la soka barani Afrika- CAF linaendelea kuchambua ni nchi gani itakayookoa jahazi ya kuwa mwenyeji wa michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon mwakani baada ya kuthibitisha Morocco kuondolewa rasmi kuandaa fainali hizo. Nchi ya Morocco imeondolewa kutokana na kukataa kuwa mwenyeji ya mashindano hayo mwakani kwa hofu ya ugonjwa wa Ebola. Kumekuwa na tetesi kuwa michuano hiyo inaweza sasa kupelekwa Angola nchi ambayo ilikuwa mwenyeji wa michuano hiyo miaka minne iliyopita. Nchi nyingine zinazodhaniwa kuweza kuandaa michuano hiyo Gabon na Nigeria na CAf inatarajiwa kutoa uamuzi wake mapema iwezekanavyo.
No comments:
Post a Comment