MSHAMBULIAJI wa klabu ya Manchester City, Edin Dzeko anakabiliwa na hatari ya kukaa nje ya uwanja kwa muda baada ya kuumia vibaya msuli wa kigimbi katika mguu wake wa kulia. Daktari wa timu ya taifa ya Bosnia-Herzegovina Reuf Karabeg amesema Dzeko mwenye umri wa miaka 28 anatarajiwa kukosa mchezo wa kufuzu michuano ya Ulaya mwaka 2016 dhidi ya Israel. Karabeg alikaririwa akidai kuwa nyota huyo ameumia vibaya na atahitaji matibabu ambayo yatachukua muda mpaka kuja kupona. Dzeko amefunga mabao manne katika mechi 17 katika kikosi cha City msimu huu lakini mpaka sasa ameshacheza mechi nane bila kufumania nyavu.
No comments:
Post a Comment