Tuesday, November 11, 2014

GREAVES AAMUA KUIPIGA MNADA MEDALI YAKE.

MCHEZAJI aliyesahaulika katika kikosi cha Uingereza kilichonyakuwa taji la michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1966, anatarajiwa kuipiga mnada medali ambayo mashabiki walimpigia debe kuipata kwa zaidi ya miaka 40. Mchezaji huyo Jimmy Greaves mwenye umri wa miaka 74 ambaye hakucheza katika mchezo wa fainali, ameamua kuiuza medali yake hiyo ya dhahabu ikiwa imepita miaka mitano toka aipokee. Kitu kingine cha kihistoria ambacho kitauzwa ni medali ya Kombe la FA ya Sir Stanley Matthew ambayo aliipata wakati Blackpool ilishinda michuano hiyo mwaka 1953. Greaves ambaye enzi aliwahi kuzichezea klabu za Tottenham Hotspurs, Chelsea na West Ham United alikosa mchezo fainali hiyo kutokana na majeruhi aliyokuwa amepata katika mechi za mwanzo. Kutokana na sheria za kipindi hicho ambazo zilikuja kubadilishwa mwaka 1974, medali hutolewa kwa wachezaji 11 pekee waliocheza mpaka dakika ya mwisho katika mchezo wa fainali.

No comments:

Post a Comment