KOCHA wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, Sven-Goran Eriksson ametangazwa kuwa kocha mpya wa klabu ya Shanghai SIPG. Eriksson raia wa Sweden alitambulishwa rasmi na maofisa wa klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya China baada ya kuzagaa tetesi kufuatia kuondoka katika timu ya Guangzhou R&F wiki iliyopita. Kocha huyo aliwaambia wana habari kuwa anafurahi hatimaye kuteuliwa kuwa kocha mpya wa klabu hiyo na hana shaka na changamoto yake hiyo mpya. Klabu ya Shanghai SIPG ambayo inatoka katika mji mmoja na timu zingine za Ligi Kuu Shanghai Shenhua na Shanghai Shenxin, inatarajiwa kuimarika zaidi chini Eriksson. Eriksson ambaye alijiunga na Guangzhou Juni mwaka uliopita alifanikiwa kuiwezesha timu hiyo kumaliza katika nafasi ya tatu katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Asia msimu huu.
No comments:
Post a Comment