Tuesday, November 18, 2014

RONALDO SASA AHAMISHIA NGUVU ZAKE KATIKA KUPINGA EBOLA.

WACHEZAJI nyota wa kimataifa wameungana na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF na wataalamu wa afya kuongeza ufahamu na kuhamasisha hatua rahisi za kuzuia katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ebola. Kampeni hiyo inayojumuisha nyota kadhaa wakiwemo Cristiano Ronaldo wa Real Madrid, Neymar wa Barcelona, Didier Drogba wa Chelsea na Philipp Lahm wa Bayern Munich inahamasisha njia 11 rahisi za ujumbe zilizochaguliwa kwa msaada wa madaktari na wataalamu wa afya kutoka Afrika, Benki ya Dunia na Shirika la Afya Duniani ambao wanapigana na ugonjwa Afrika Magharibi. Chini ya kauli mbiu inayoitwa Kwa Pamoja Tunaweza Kutokomeza Ebola, wachezaji hao wamekuwa wakituma ujumbe kwa njia ya sauti, picha za video na ujumbe wa maneno kuelekea kwa mashabiki wao kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii. Ofisa mkuu wa afya wa FIFA Profesa Jiri Dvorak amesema wao wakiwa kama madaktari wameona nguvu ya mchezo wa soka wakati linapokuja suala la kuzuia na afya ndio maana wameamua kutumia mfumo huo ili kupambana na Ebola. Naye rais wa FIFA Sepp Blatter amesema umaarufu wa mchezo wa soka unawapa nafasi ya kipekee kufikia jamii zote hivyo ni matumaini yao kampeni zilizoanzishwa dhidi Ebola zitaongeza uelewa kwa jamii husika ili kupunguza maambukizi. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Shirika la Afya Duniani-WHO mpaka kufikia Novemba 9 mwaka huu, jumla ya watu wapatao 14,098 walithibitika kuambukizwa ugonjwa huo katioka nchi sita tofauti zaidi ikiwa nchi za Guinea, Kiberia na Sierra Leone huku wengine 5,160 wakiwa wamepotyeza maisha.

No comments:

Post a Comment