Tuesday, November 18, 2014

GIGNAC AZUA KIZAAZAA MARSEILLE.

RAIS wa klabu ya Olympique de Marseille Vincent Labrune anashikiliwa kwa mahojiano kuhusiana na uchunguzi wa uhamisho wa mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Andre-Pierre Gignac. Labrune alihojiwa jijini Marseille na mkurugenzi mtendaji wa timu hiyo Philippe perez wakati rais wa zamani Jean-Claude Dassier yeye alikuwa akihojiwa katika mji wa Nanterre uliopo nje kidogo ya jiji la Paris. Wapelelezi wanajaribu kuona kama maofisa hao w klabu kamisheni isivyo halali wakati Gignac aliposajiliwa akitokea Toulouse mwaka 2010. Marseille kwasasa wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu ya Ufaransa baada ya kucheza mechi 13 huku Gignac akiwa amefunga mabao 10.

No comments:

Post a Comment