KIUNGO mahiri wa klabu ya Borussia Dortmund, Nuri Sahin amethibitisha mwenyewe kuwa fiti kwa ajili ya kurejea uwanjani baada ya kupona majeruhi yaliyokuwa yakimsumbua. Nyota huyo wa kimataifa wa uturuki alikosa maandalizi yote ya msimu kabla ya kufanyiwa upasuaji kufuatia matatizo ya goti huku mchezo wake wa mwisho wa mashindano ukiwa wa fainali ya Kombe la Ujerumani Mei mwaka huu. Hata hivyo, Sahin mwenye umri wa miaka 26 sasa anakaribia mwishoni kupona huku akikiri hasikii maumivu yeyote na anahitaji kurejea uwanjani haraka iwezekanavyo. Sahin aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii kuwa anatamani kurejea tena uwanjani baada ya maumivu aliyokuwa akisikia kuondoka.
No comments:
Post a Comment