Tuesday, November 18, 2014

MWENYEKITI WA FA ATAKA RIPOTI KAMILI YA GARCIA.

MWENYEKITI wa Chama cha Soka cha Uingereza-FA, Greg Dyke amewaandikia barua maofisa watendaji wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA akitaka taarifa kuhusiana na tuhuma za rushwa Kombe la Dunia kutolewa yote kama ilivyowasilishwa. Kurasa 42 zilizohaririwa zilitolewa wiki iliyopita lakini haraka ilikosolewa na Michael Garcia ambaye alitumia muda wa miaka miwili kufanyia uchunguzi tuhuma hizo za rushwa. Katika barua yake Dyke anataka ripoti iliwasilishwa na Garcia kutolewa bila kuhaririwa ili kuona yaliyokuwemo humo. Garcia anatarajiwa Alhamisi kukutana na jaji wa kamati ya maadili ya FIFA Hans-Joachim Eckert ambaye alitoa taarifa hiyo iliyohaririwa wiki iliyopita ili kujadili masuala ambayo anayakosoa. Dyke amesema kushindwa kutolewa kwa ripoti ya Garcia kunapunguza imani na shirikisho hilo na ili wajisafishe ni lazima waitoe ili waliohusika waashughulikiwe.

No comments:

Post a Comment