SHIRIKISHO la Soka la Croatia limethibitisha kuwa majeruhi aliyopata kiungo wa Real Madrid Luka Modric yatamuweka nje ya uwanja mpaka Februari mwakani. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 alipata majeruhi hayo katika kipindi cha kwanza cha mchezo wa kufuzu michuano ya Ulaya mwaka 2016 kati ya Italia na Croatia mbao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1. Modric alitolewa nje na kwenda kufanyiwa vipimo jijini Madrid ambapo majibu yake yameonyesha atakaa nje kwa muda wa miezi mitatu. Katika taarifa yake shirikisho hilo lilidai kuwa nyota huyo hatahitaji upasuaji kwani tatizo lake litakwisha kwa matibabu ya kawaida. Modric sasa anatarajiwa kukosa michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia itakayofanyika nchini Morocco mwezi ujao.
No comments:
Post a Comment