KOCHA wa timu ya taifa ya Ureno Fernando Santos amedokeza kuwa Cristiano Ronaldo ndio mwenye nafasi ya kushinda tuzo ya Ballon d’Or na kukiri kuwa amempigia kura nahodha wake huyo badala ya Lionel Messi. Ureno ina alama sita katika mechi zao tatu za kufuzu michuano ya Ulaya mwaka 2016 walizocheza mpaka sasa baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya Armenia Ijumaa iliyopita huku wakikabiliwa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Argentina baadae leo. Mchezo huo ni nafasi nyingine kuona Ronaldo akichuana na hasimu wake Messi ambapo safari hii watavaana katika Uwanja wa Old Trafford jijini Manchester. Akihojiwa Santos alikiri kumpigia kura Ronaldo kwani anadhani msimu huu ndiye mchezaji bora wa dunia lakini pia hakuacha kusifia na ubora wa Messi.
No comments:
Post a Comment