Thursday, November 20, 2014

ALIYEFICHUA SIRI KUHUSU QATAR KUTOA HONGO AHOFIA MAISHA YAKE.

ALIYEFICHUA siri kuhusu tuhuma za rushwa kutolewa na Qatar ili kuiwezesha nchi hiyo kushinda nafasi ya kuandaa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022 ameiambia BBC kuwa anaishi kwa hofu kutokana na hatua yake hiyo. Mwaka 2011, Phaedra al-Majid alidai kuwa maafisa wa Qatar walijitolea kuwalipa maafisa watatu wa vyama vya soka barani Afrika kiasi cha dola milioni moja na nusu ili kuiunga mkono Qatar kuwa mwenyeji wa michuano hiyo mikubwa duniani. Baadaye Bi Phaedra al-Majid aliondoa tuhuma hizo, lakini sasa anasema alilazimishwa kubadili kauli yake. Amesema ameingia katika hali ya kutojitambua na kuona anaonewa kila wakati, hofu na vitisho na kudai atajiona atajiona mkosaji maisha yake yote. Kamati ya Qatar ya uandaaji wa mihuano hiyo imesema ushahidi wa Phaedra al-Majid ulitiliwa mashaka na timu ya uchunguzi ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, na kwamba tuhuma zote zilichunguzwa na kutupiliwa mbali.

No comments:

Post a Comment