Thursday, November 20, 2014

NYOTA WA NBA AFUNGIWA MECHI 24 KWA KUMPIGA MPENZI WAKE.

MCHEZAJI nyota wa mpira wa kikapu wa timu ya Charlotte Hornets Jeffery Taylor amefungiwa kucheza mechi 24 bila kulipwa baada ya kukutwa na hatia ya kudhalilisha. Kwa mujibu wa taarifa za polisi Taylor alionekana akimbamiza rafiki wake wa kike ukutani na kumpiga mkononi. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 tayari ameshakosa michezo 11 kutokea kuanza kwa msimu lakini alikuwa akilipwa hivyo sasa ataendelea kukosa mshahara mpaka atakapomaliza adhabu yake. Kamishna wa Ligi ya Mpira wa Kikapu Marekani-NBA, Adam Silver amesema matukio kama hayo yanatia doa ligi hiyo.

No comments:

Post a Comment