Thursday, November 20, 2014

SWANSEA YAMUONGEZA MKATABA WA MWAKA MMOJA BONY.

KLABU ya Swansea City imetangaza kumuongeza mkataba wa mwaka mmoja mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast Wilfried Bony. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 sasa ataendelea kusalia Swansea mpaka mwaka 2018. Bony amekuwa akihusishwa na tetesi za kuondoka Swansea huku vilabu vya Liverpool, Arsenal na Tottenham Hotspurs zikitajwa kutaka kumsajiali. Meneja wa Swansea Garry Monk amesema amefurahishwa kumbakisha nyota huyo kwani amekuwa sehemu muhimu katika kikosi chake hicho. Bony ambaye aliiongoza Ivory Coast katika michuano ya Kombe la Dunia June mwaka huu, amefunga mabao 25 akiwa na Swansea msimu uliopita huku akifunga mengine manne katika mechi 11 msimu huu.

No comments:

Post a Comment