Thursday, November 20, 2014

ALIYEJITANGAZA SHOGA NBA ASTAAFU.

MCHEZAJI wa kwanza aliyejitangaza kuwa shoga katika Ligi ya Mpira wa Kikapu nchini Marekani Jason Collins ametangaza kustaafu rasmi mchezo huo. Collins mwenye umri wa miaka 35 alijitangaza kuwa ni shoga wakati akiichezea timu ya Brooklyn Nets msimu uliopita. Nyota huyo ambaye hakujumuishwa katika kikosi cha msimu huu amesema mwili wake umeshafikia hatua ya mwisho ndio maana ameamua kuchukua hatua hiyo ngumu. Kabla ya kustaafu Collins amecheza NBA kwa kipindi cha miaka 13 kabla ya kujitangaza shoga Aprili mwaka jana. Collins amesema anadhani kwasasa atabakia mshabiki wa mchezo huo ambao amekuwa akiupenda katika maisha yake.

No comments:

Post a Comment