Thursday, November 20, 2014

KOCHA WA TOGO AKUBALIA KUSHINDWA.

KOCHA wa timu ya taifa ya Togo, Tchakala Tchanile amekiri kuwa timu yake walifungwa na timu bora baada ya kupokea kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Ghana katika mchezo wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika mwakani. Kiwango cha chini kilichoonyeshwa na Togo katika mchezo huo uliofanyika huko Tamale mji uliopo kaskazini wa Ghana ulipelekea kuipa nafasi Black Stars kujikatia tiketi ya kushiriki michuano hiyo. Tchanile alikipongeza kikosi cha Ghana kwa mchezo mzuri na kuonyesha nia ya kupambana kuanzia mwanzo wa mchezo mpaka mwisho. Kocha huyo amesema Ghana walionekana toka mwanzo kuwa wanataka kushinda katika mchezo huo na anadhani wachezaji wote 11 uwanjani walifanya juhudi kuhakikisha wanashinda. Kwa matokeo hayo Togo imeshindwa kufuzu michuano hiyo itakayofanyika mwakani huko Guinea ya Ikweta.

No comments:

Post a Comment