Tuesday, November 4, 2014

KOCHA WA VITA AAPA KUPAMBANA ILI AWEZE KUREJEA TENA KATIKA MICHUANO HIYO MWAKANI.

BAADA ya kupoteza taji la Ligi ya Mabingwa Afrika kwa timu ya Entente Setif ya Algeria, kocha wa Vita Club Florent Ibenge amesema kikosi chake kitaendelea kupambana na kuhakikisha wanarejea tena katika michuano hiyo mwakani. Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilipoteza taji hilo muhimu baada ya kutoa sare ya mabao 3-3 dhidi ya Setif na kujikuta wakishindwa kwa tofauti ya mabao ya ugenini. Hata hivyo, wachambuzi wa soka wameipongeza Vita kwa kuonyesha mchezo wa kiwango cha juu dhidi ya Setif ambao walikuwa wakipewa nafasi ya kubwa ya kutamba katika fainali ya mkondo wa pili baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa kwanza. Ibenge amesema walijitahidi kadri wawezavyo kuonyesha soka safi zaidi ya walivyofanya katika mchezo wa nyumbani Kinshasa lakini umaliziaji haukuwa mzuri. Vita waliambulia kitita cha dola milioni moja wakati mabingwa Setif wao walikunja kitita cha dola milioni 1.5 pamoja na tiketi ya kushiriki michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia.

No comments:

Post a Comment