MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amebainisha kuwa klabu hiyo iko katika majadiliano na Theo Walcott kuhusiana na mkataba mpya. Walcott alijiunga na klabu hiyo mwaka 2006 akitokea Southampton na Jumamosi iliyopita alirejea tena uwanjani katika mchezo dhidi ya Burnley baada ya kukaa nje kwa kipindi cha miezi tisa kutokana na majeruhi ya goti. Nyota huyo alisaini mkataba wa miaka miaka mitatu na nusu Januari mwaka jana, mkataba ambao utamalizika kiangazi mwaka 2016. Wenger amesema tayari wameanza kufanya naye mazungumzo na anadhani mambo yote yataweza kwenda sawa.
No comments:
Post a Comment