KOCHA wa timu ya taifa ya Sweden, Erik Hamren amemuita majeruhi Zlatan Ibrahimovic katika kikosi chake ambacho kinakabiliwa na mchezo wa kufuzu michuano ya Ulaya mwaka 2016 dhidi ya Montenegro na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Ufaransa. Ibrahimovic hajacheza toka Septemba 21 kwasababu ya matatizo ya kisigino lakini kocha wa klabu ya Paris Saint-Germain Laurente Blanc alidai wiki iliyopita kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 33 yuko njiani kupona. Katika taarifa ya Shirikisho la Soka la Sweden, wamedai kuwa ushiriki wa mchezaji huo utategemea kupona kwake majeruhi yanayomsumbua. Hamren amesema anatumaini mchezaji huyo ataanza mazoezi wiki hii na kuitumikia PSG kabla ya mchezo wao kufuzu. Sweden wanashika nafasi ya tatu katika kundi G wakiwa wamejikusanyia alama tano katika mechi tatu.
No comments:
Post a Comment