Wednesday, December 17, 2014

ABIDAL AJIPANGA KUSTAAFU.

BEKI wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa, Eric Abidal jana amecheza mchezo wake wa mwisho akiwa na klabu ya Olimpiakos katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Uturuki dhidi ya Panionios ambao walishinda kwa mabao 2-0. Kocha wa Olimpiakos Michel alithibitisha mara baada ya mchezo huo kuwa ulikuwa wa mwisho kwa Abidal mwenye umri wa miaka 35 ambaye anatarajiwa kutangaza kustaafu rasmi kesho. Michel amesema Abidal alishatoa uamuzi huo wa kuondoka Olimpiakos miezi miwili iliyopita na anajivunia kupata nafasi ya kumfundisha nyota huyo. Abidal aliwahi kufanyiwa upasuaji wa kupandikiza ini lingine kabla ya kurejea tena katika ulimwengu wa soka akiwa na klabu ya Barcelona. Aliondoka Barcelona mwaka jana baada ya kupona upasuaji aliofanyiwa na kuhamia klabu yake ya utotoni ya Monaco ya Ufaransa.

No comments:

Post a Comment