BINGWA wa dunia wa zamani anayeshikilia rekodi katika mbio za marathon, Wilson Kipsang amelituhumu Shirikisho la Riadha la Kenya-RK kwa kumharibia jina lake kwa kumtuhumu kushindwa kufanyiwa vipimo vya dawa za kusisimua misuli. Shirikisho la Riadha la Kimataifa-IAAF liliiambia RK kuwa walijaribu kumfanyia vipimo Kipsang Novemba 11 mwaka huu. Kipsang mwenye umri wa miaka 32 amesema ni kweli alikosa kufanyiwa vipimo katika siku hiyo aliyopangiwa na IAAF lakini alikuwa katika majukumu mengine na aliwasilisha nyaraka zote zinazohitajika. Mwanariadha huyo amesema analifuatilia kwa undani suala hilo pamoja na wanasheria wake waone kama wanaweza kufungua kesi kwa RK kumharibia jina lake.
No comments:
Post a Comment