Wednesday, December 17, 2014

WAZIRI ALGERIA AWATAKA MASHABIKI KUTOSAFIRI NA TIMU.

WAZIRI wa michezo wa Algeria amewataka mashabiki wa soka wa timu ya taifa ya nchi hiyo kutosafiri kwa ajili ya kushuhudia michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon itakayoanza mapema mwakani huko Guinea ya Ikweta. Mji wa Mangomo ambao Algeria ndio watacheza mechi zao za makundi dhidi ya Afrika Kusini, Ghana na Senegal una hoteli chache zenye hadhi na zote kati ya hizo zimechukuliwa na timu za taifa. Waziri huyo Mohammed Tahmi amesema mazingira hayaridhishi katika mji huo wa Mangomo ndio maana amewatahadharisha mashabiki mapema. Tahmi aliendelea kudai kuwa mashabiki watakaokwenda Guinea ya Ikweta watapata tabu kutoka upungufu wa hoteli hali ambayo inaweza kuwaathiri pia hata waandishi wa habari watakaokwenda huko. Zaidi ya mashabiki 2,500 walisafiri kuifuata Algeria katika michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika nchini Brazil.

No comments:

Post a Comment