MENEJA wa klabu ya Manchester City, Manuel Pellegrini amesema Sergio Aguero ni moja kati ya wachezaji watano bora duniani baada ya ushindi wa mabao 4-1 iliyopata timu yake dhidi ya Sunderland jana. Katika mchezo huo City walitoka nyuma na kufanikiwa kushinda mchezo huo muhimu na kumfanya Aguero kufikisha jumla ya mabao 14 msimu huu. Pellegrini amesema anadhani Aguaero yuko katika orodha ya wachezaji watano bora duniani na kwa umri wa miaka 26 alionao bado ana nafasi ya kuimarika zaidi. Mbali na Aguero, kocha huyo pia aliwapongeza viungo wake Yaya Toure na Samir Nasri kwa juhudi zao kubwa kuhakikisha wanajiimarisha katika nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu.

No comments:
Post a Comment